Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wana bahati ya kukutana na vibonde - Mchambuzi

Yanga Vs Merrikh 2 0.jpeg Wachezaji wa Yanga wakishangilia

Sun, 17 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa TV3 Alex, Ngereza amedai kuwa timu ya soka ya Yanga SC imekuwa kikikutana na vibonde kwenye mashindano ya CAF ndiyo maana inashinda kirahisi na kufanya kufanya vizuri.

Ngereza amesema hayo mara baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Al Merrikh ya Sudan kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa uliopigwa katika Dimba la Kigali Pele, Rwanda jana Jumamosi.

Kabla ya mchezo huo, Yanga ilikutana na ASAS FC ya Djibouti ya kuifunga jumla ya bao 7-1 katika michezo miwili.

Ikumbukwe pia kuwa Msimu uliopita Yanga iliifunga Zalan FC ya Sudan Kusini mabao 9 kwenye michezo miwili kabla ya kutolewa na Al Hilal na kuangukia Kombe la Shirikisho ambapo Yanga ilicheza mpaka hatua ya fainali.

"Yanga wana bahati ya kukutana na Vibonde tangu msimu uliopita kwenye kombe la shirikisho barani Africa na msimu huu kwenye club bingwa barani Africa kwenye hizi hatua za awali

MSIMU ULIOPITA

"YANGA vs Mazembe alikuwa dhofuli hali yanga wakashinda kirahisi tu

"YANGA VS Us Monastiry ilikuwa mara yake ya kwanza kushiriki makundi tofauti na Yanga ambayo ilikuwa inashiriki kwa mara tatu

"YANGA VS Real Bamako ni timu ambayo tayari ilishajichokoea toka mda mrefu ndio maana Yanga walipata matokeo kirahisi sana

"YANGA vs Rivers hii timu ilikuwa inaingia robo fainali kwa mara ya kwanza na hata makundi ilikuwa ni mara yake ya kwanza tofauti na Yanga ambao walikuwa na uzoefu mkubwa kwenye kombe la shirikisho

"YANGA vs Marumo Gallants wao walikuwa wameshuka daraja kabisa kwahio ilikuwa bahati nyingine kwa Yanga ndio maana hata kushinda ikawa rahisi sana

MSIMU HUU

"YANGA VS ASAS..hapa Yanga walipata bahati nyingine ya kukutana na timu ambayo haina ubora na wakapata bahati ya kucheza mechi zote mbili nyumbani na ugenini wakapata matokeo mazuri

"YANGA VS El Merrick hii bahati nyingine kwa Yanga wamekutana na timu ambayo haina ubora imebaki na historia yake tu ndio maana wamepata matokeo kirahisi sana.

"El Merrick wamechoka kiaina kwahio Yanga wasijisifie sana tusubiri kwenye hatua ya makundi ndio wataenda kukutana na timu bora zenye wachezaji bora kama wao ndio tutaona kweli yaliomo yamo au itakuwaje," amesema Alex Ngereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live