Desemba 2, 2023, Yanga SC atampokea bingwa mtetezi wa ligi ya Mabingwa Afrika Al Ahly ambaye mchezo wa kwanza dhidi ya Madeama ameshinda na Yanga akipoteza mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya CR Belzoudad.
Lakini roundi hii Yanga yupo uwanja wa Nyumbani Mkapa uwanja ambao msimu uliopita kwenye kombe la shirikisho alishinda michezo yote lakini kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa hatua ya makundi Yanga anawastani mzuri wa kushinda uwanja wa Nyumbani je kuendeleza ubabe wake?
YANGA SC 1-1 MANNING RANGERS YANGA SC 3-3 RAJA CASABLANCA YANGA SC 0-3 ASEC MIMOSAS YANGA SC 1-0 TP MAZEMBE YANGA SC 1-1 MADEAMA YANGA SC 1-0 MO BEJAIA YANGA SC 0-0 RAYON SPORTS YANGA SC 2-3 GOR MAHIA YANGA SC 2-1 USM ALGER YANGA SC 3-1 TP MAZEMBE YANGA SC 2-0 REAL BAMAKO YANGA SC 2-0 US MONASTIR
Mara ya mwisho Yanga kukutana na Al Ahly ilikuwa ni mwaka 2016 katika hatua ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa ambapo Yanga ilitoa sare ya bao 1-1 nyumbani kisha ikaondolewa kwa kufungwa bao 2-1 ugenini, bao la Yanga likifungwa na Donald Ngoma.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2014, Yanga iliwahi kuifunga bao 1-0 kwenye michuano ya CAF Champions League. Yanga pia imewahi kupokea kipigo cha bao 5-0 kutoka kwa Ahly mwaka 1982.
Katika mechi 10 za mwisho walizokutana, Yanga imeshinda mechi moja, imeota sare 3 na kupoteza michezo 6.
Je kwa kiwango cha Sasa Cha Yanga SC na Al Ahly unaona mechi kwa Mkapa Wananchi watafanikiwa kuondoka na alama tatu?