Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamuandalia Ibenge dakika 90 za moto Sudan

Yanga Players Wachezaji wa Yanga wakiendelea kujifua Avic Town

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: mwanaspoti

Yanga juzi walirejea mazoezini na safari hii wakianzia gym kujiweka sawa miili yao tayari kupindua meza dhidi ya Al Hilal nchini Sudan na kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mastaa wa zamani wa Yanga wamewapa gia mpya ya kufuta sare ya bao 1-1 na kufuzu kuondoa unyonge wa mashabiki wao ambao wameonekana kujawa na wasiwasi.

Chini ya kocha mkuu Nasreddine Nabi, mastaa hao wa zamani wanaamini Yanga inapaswa kushambulia na kujiamini tu kinyume cha hapo hawawezi kupata ushindi wa ugenini.

Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alishauri mastaa wa Yanga kujitoa mhanga, kujiamini, kuweka dhamira ya kuamini hakuna kinachoshindikana kuwania ushindi ndani ya dakika 90 ili mradi kila timu inaingiza wachezaji 11.

“Morali na hamasa ambayo ilikuwepo kwa mashabiki, makocha, viongozi na wachezaji ya kupata ushindi mechi iliyochezwa kwa Mkapa ndiyo hiyo hiyo iendelee kwenye mchezo wa marudiano, kwani kila timu itaingiza wachezaji 11, hilo likamfanye kila mchezaji kusimamia majukumu yake ya kuibeba timu,”alisema.

Veterani wa Simba, Mohamed Banka alisema; “Uzalendo kwa maana ya kila mchezaji akaiweke Yanga mbele kabla ya maslahi yake watakwenda kufanya vitu kikubwa, ninachotamani nikuona timu za Tanzania zinacheza kwa kiwango kikubwa ili kuendelea kukuza thamani ya soka letu, wakijiandaa watashinda.”

Alisema kama Simba imeweza kushinda Angola, aliona basi Yanga ichukue kama funzo la ujasiri na kunia mamoja kwamba lazima Sudan wakakiwashe na kuacha historia ya kuwapa kichapo Al Hilal kwenye uwanja wao.

Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ fundi wa zamani wa kupachika mabao ndani ya kikosi hicho, alisema; “Yanga ina kikosi, wakaingie uwanjani kwa kushambulia na kujiamini, wakifanya hivyo naamini watabadilisha upepo, tofauti na sasa ambapo mashabiki wengi wamekata tamaa.”

Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze ambaye moja kati ya majukumu yake mnakubwa kikosini ni kuusoma mchezo ujao na kumshauri bosi wake alikiri kuona udhaifu kwenye mechi hiyo akasema; Ni kweli siyo kazi nyepesi, lakini tupo imara kwenda kupigania ushindi ugenini, kama wao wameweza kupata bao kwetu sisi tutashindwaje kwao, siyo kazi nyepesi ila tunakwenda kushindana na tunaamini sisi ni washindi.”

TAKWIMU ZAO

Hilal wamekuwa rekodi nzuri nyumbani, katika mechi 10 za mwisho, Wasudan hao wamepoteza mara moja tu ambapo ilikuwa Machi 19, 2022 kwa mabao 4-2 dhidi ya miamba ya soka la Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns.

Al Hilal imeibuka na ushindi mara nne huku ikitoka sare tano ambazo ni dhidi ya TP Mazembe (0-0), Belouizdad (0-0), Mamelodi Sundowns (0-0), Fasil Kenema (1-1) na Al Ahly (0-0). Yanga imepania kufuzu hatua ya makundi pamoja na kutetea vikombe vyake kwenye ligi za ndani.

Chanzo: mwanaspoti