Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamuaga Magufuli

D7a4b0bd73b55bdd3c2b388c2067cf26 Yanga wamuaga Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Mshindo Msola ameongoza msafara wa viongozi na wachezaji wa timu hiyo kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 Dar es Salaam.

Yanga watamkumbuka Magufuli kwa mengi aliyoyafanya kwa klabu hiyo katika kipindi chake ikiwamo kupata eneo la ujenzi wa uwanja Kigamboni pamoja na kushinda taji la Mapinduzi katika kipindi cha uongozi wake ambalo mara ya mwisho walitwaa mwaka 2007.

Wana Jangwani hao walikuwa kambini huko Kigamboni, lakini jana walikatisha ratiba yao ya mazoezi na kuamua kwenda kumuaga Hayati Magufuli katika Uwanja wa Uhuru uliopo wilaya ya Temeke, Dar es Salaam.

Yanga waliaga mwili huo majira ya saa 4:04 asubuhi wakiongozwa na Msola, akifuatiwa na mshauri wa klabu hiyo, Senzo Mbatha raia wa Afrika Kusini na baadaye Katibu Mkuu, Haji Mfikirwa na kocha wa muda wa kikosi hicho, Juma Mwambusi ambaye alikuwa mbele ya Meneja, Hafidh Saleh.

Msafara huo uliokuwa na nyota kama Farouk Shikhalo, Ramadhan Kabwili, Paul Godfrey, Kibwana Shomari, Adeyun Saleh, Lamine Moro, Said Juma Makapu na Abdallah Shaibu Ninja.

Wengine ni Zawadi Mauya, Haruna Niyonzima, Tuisila Kisinda, Waziri Junior, Yacouba Songne, Michael Sarpong na Fiston Abdul Razack.

"Kama klabu tumetoa heshima yetu kwa Hayati Rais John Magufuli ambaye wakati wake wa uongozi alikuwa mpenda michezo," alisema Dk Msolla.

Yanga imekuwa na msimu mzuri mwaka huu ambapo kwa muda mrefu imekuwa vinara wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara hadi Rais Magufuli anaaga dunia.

Bwana alitoa na Bwana na Bwana aAlitwaa, jina lake lihidimiwe. Amina.

Chanzo: www.habarileo.co.tz