Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wametimiza malengo yao, sasa wathibitishe ubora wao

Yanga Gamondi Wachezaji Yanga wametimiza malengo yao, sasa wathibitishe ubora wao

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga nafasi ya tatu kwa ubora barani afrika kwa mujibu wa Shirikisho la kimataifa la historia na takwimu za Mpira Duniani (IFFHS) pamoja na msimu uliopita walicheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Usm Alger tena wakishinda mchezo wa ugenini dhidi ya Usm Alger na katika hatua ya makundi wakishinda dhidi ya club African.

Baada ya kupangwa kwa makundi ya ligi ya Mabingwa Yanga kuwa katika kundi D na vigogo bingwa wa kihistoria Al Ahly,Belouizdad na Madeama SC ya Ghana pamoja ndiyo wakati wa kuthibitisha ubora wao kwanini wanashika nafasi ya tatu kwa ubora Afrika.

Msimu uliopita wachezaji wengi katika shirikisho walionesha quality ya Hali ya juu Sasa ni zamu ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu kuonesha ubora na makali Yao mtu kama Max Mzengeli,Pacome ,Khoausi Yao Yao,Skudu ambao wote wanauzoefu na michuano ya kimataifa.

Yanga alicheza fainali na USM Alger ambaye msimu huu katika super Cup ambayo inakutanisha bingwa wa ligi ya Mabingwa na kombe la shirikisho na USM Alger kushinda kwa bao Moja kwa sifuri ivyo Mwananchi nao wanajambo la kufanya msimu huu kuweka rekodi zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live