Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia TV3, Boiboi Mkali amesema kuwa wanachokifanya Klabu ya Yanga ni 'copy and paste' ya miamba wa soka nchini Hispania, Klabu ya Sevilla.
Itakumbukwa kuwa, Yanga waliingia mkataba na Sevilla kisha La Liga kwa ajili ya uendeshaji wa klabu hiyo na mfumo mzima wa mabadiliko ambayo mpaka sasa wapo kwenye hatua nzuri.
"Wakati Yanga inaingia mkataba na timu ya Sevilla Fc kutoka nchinia Hispania watu hawakuelewa malengo ya Yanga lakini sasa hivi tunaona faida yake.
"Sasa hivi Yanga mfumo wake ndani na nje ya uwanja ni kama timu za Hispania. Wamechukua kila kitu kutoka timu za Hispania na wanatumia mfumo huo vizuri sana," amesema Boiboi Mkali.