Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamekiheshimisha hiki kizazi

Yanga ZtR.jpeg Yanga wamekiheshimisha hiki kizazi

Tue, 8 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanakuja na kuondoka,maisha yanakuja na kupita,matukio nayo yanakuja na kuondoka huku matukio haya yakiletwa au kufanywa na watu tena watu wa wakati husika,yawe mazuri au mabaya yote kwa yote yataacha furaha au huzuni ambazo baada ya muda huzaa kumbukumbu.

Kupitia matukio ndipo alama hupatikana,ndipo heshima huongezeka ndipo tofauti baina ya watu katika jamii huonekana ndipo ukubwa halisi hupatikana pia.

Unaweza kupata matukio bora yaliyopita kwa masimulizi ya kawaida kutoka kwa shuhuda wa pembeni,kutokana na vipande vya picha au kumbukumbuku za maandishi ambazo bado haziwezi kukata kiu kama sio kukupa kitu halisi kwa ukubwa wake.

Lakini kwa kutumia sanaa na weledi wa hali ya juu kwa kuunganisha matukio yote tena kwa mpangilio sahihi katika picha au sauti au video ndipo Documentary huzaliwa, ndio uhalisia wa jambo hupatikana ndipo Yanga sc walipoweza kujitofautisha na wengine.

Documentary ni kumbukumbu halisi ni mkusanyiko wa nyakati zote,ni kitu halisi kikieleza jambo kwa ukamilifu wake.

Yanga sc wameamua kukiheshimisha kizazi hiki,wameamua kuwapendelea mashabiki wao kwa kuwapunguzia kazi ya kujieleza siku zijazo,wameamua kuwatengenezea heshima itakayodumu milele na milele hii sio kwa ajili ya wachezaji wala viongozi bali ni kwa wanayanga ambao wapo na Yanga jana,leo na hata milele.

Hizi ni kumbukumbu muhimu kwa klabu ambapo huleta chachu siku hadi siku lakini kubwa ni sehemu ya kujenga uchumi wa klabu kwani kila utakapotaka kuingalia kupitia AZAM MAX na official app zinginge kwa kuchangia gharama ndogo ya Tsh.2500/= utaweza kujionea yote mazuri na magumu ya msimu uliopita lakini pia utakua umechangia timu yako pendwa.

Hili ni jambo kubwa ni wakati wa kulitazama kwa ukubwa wake Viongozi wenu chini ya Rais wenu Eng.Hersi Said wameamua kuwaheshimisha kama sio kuwatofautisha na wengine, sasa kwanini msiwashukuru kwa kulichangamkia jambo hili?kama mliweza kuweka rekodi ya kucheza fainali ya shirikisho kwanini msiweke rekodi ya mapato kupitia kuitazama Documentary hii kupitia AZAM MAX?" Dominick Salamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live