Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamefanya jambo la kiungwana kwa Mayele

Mayele Hdfsgs.jpeg Yanga wamefanya jambo la kiungwana kwa Mayele

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imekubali kumuuza mshambuliaji wao tegemezi Fiston Mayele kwenye timu ya Pyramids kutoka Misri.

Hiki ni kitendo cha uungwana sana, kukubali kumruhusu Mayele aondoke kwa amani bila mvutano wala marumbano yoyote, japo alikuwa na mkataba wa mwaka moja na Yanga SC.

Yanga walikuwa na uwezo wa kumbakiza klabuni hapo kwa nguvu na angeendelea kusalia Yanga kwa mwaka moja, lakini hawajafanya hivyo.

Ikumbukwe Yanga ndio timu iliompatia Mayele jina kubwa, kuitwa kwenye timu ya Taifa ya Congo DR, kuhitajika pia na klabu kubwa kama Pyramids.

Hakika Yanga sc ndio daraja la mafanikio ya Mayele huko aendako, na huo ndio uungwana. Pole za dhati kwa mashabiki wa Yanga kwani hii taarifa sio nzuri kwao. Lakini maisha lazima yaendelee. Kila la kheri Fiston Mayele huko Pyramid.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: