Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wameanza kujiona Man City

Yanga Algeria Tiziiiiii Yanga wameanza kujiona Man City

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Najua kama Yanga wamewahi kufungwa mpaka 5-0 huko nyuma lakini, sikumbuki mara ya mwisho walipofungwa 3-0! Baada ya miaka takribani 25 bila kucheza hatua ya Makundi Klabu Bingwa Afrika, nilidhani Yanga wana Adabu.

Baada ya kutoshiriki kwa miaka mingi, nilidhani Yanga wamekuwa na heshima kubwa sana kwa wapinzani, kumbe wapi! Bado Yanga ni jeuri. Bado Yanga ni watu wa misimamo. Bado Yanga inaamini inaweza kucheza na timu yoyote duniani na kushinda. Yanga haina heshima iwe ugenini au nyumbani. Yanga haina heshima ama iwe inacheza mechi za ligi Kuu Tanzania Bara au Klabu Bingwa Afrika. Ukiniuliza ni Kwanini Yanga walimfungwa mabao 3-0 kule nchini Algeria Wikiendi iliyopita dhidi ya CR Belouizdad, nitakwambia Yanga hawana adabu. Kwa mtu ambaye alitazama mpira, ni vigumu sana kuelewa ni kwanini Yanga walifungwa goli nyingi kiasi hicho wakati alitawala karibu kila kitu. Tangu Yanga walivyotwaa ubingwa wa ligi mara mbili mfululizo, tangu Yanga walivyocheza fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kwa sasa wanadhani wao ni kama Manchester City.

Kuna namna wanajiona kama wameshakuwa sawa na Real Madrid! Mpira unataka adabu. Unataka mipango ya kumuheshimu mpinzani. Unataka mipango ya kujua mapungufu yako. Yanga kujiamini kumepitiliza. Tangu wamfunge Simba 5-1, wanaona kila timu kwao haitoboi.

Uzuri wa mpira ni mchezo wa wazi na kila mtu anaona. Najua na wewe ulipata nafasi ya kuutazama mchezo na una maoni yako. Ni kweli Yanga walikosa adabu dhidi ya CR Belouizdad? Naomba maoni yako kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba Yangu ya simu hapo juu.

Mechi dhidi ya CR Belouizdad, Yanga walikosa tu adabu kwa mpinzani. Walicheza kama wanavyocheza na KMC. Walikuwa ni kama wanacheza na timu kutoka Djibout! Mpira unataka sana kumjua mpinzani wako na usijiamini kupitiliza.

Yanga bado hana rekodi nzuri sana kihistoria kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika. Bado sana. Yanga ni Wafalme wa Soka la ndani. Unapokwenda “Kimataifa “, unahitaji kuwa na Adabu. Yanga alitawala sana mchezo, lakini CR Belouizdad wao walitawala sana Matokeo.

Hawakuwa na tabu Yanga kumiliki mpira. Hawakuwa na tabu Yanga kuupiga mwingi, lakini walihakikisha Yanga hapati goli. Karibu kila shambulizi la kushitukiza walilofanya lilileta bao. Yanga wanajikita wako pungufu na wanafungwa kirahisi. Karibu kila mchezaji wa Yanga kule Algeria alikuwa anataka kufunga bao. Hata mabeki wao nao walikuwa wanaona wanajukumu la kwenda mbele na kufunga! Ukikosa adabu uwanjani, utaadhibiwa tu.

Ni vizuri kujiamini lakini kusipitilize. Ukiniuliza ni kwa nini Yanga ilifungwa mabao mengi Wikiendi iliyopita kule nchini Algeria, nitakujibu walikosa adabu kwa mpinzani wao. Walijiamini kupitiliza. Uzuri wa mpira ni mchezo wa wazi na kila mtu anaona. Najua na wewe ulipata nafasi ya kuutazama mchezo na una maoni yako.

Ni kweli Yanga walikosa adabu dhidi ya CR Belouizdad? Naomba maoni yako kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo Juu.

Yanga wanapaswa kuwa na adabu hasa wanapocheza na timu zenye historia na rekodi kubwa Afrika kuliko wao. Sio kila timu ni TP Mazembe. Ni kweli Yanga wana timu nzuri. Ni kweli Yanga wametoka kushinda mechi zao sita mfululizo za ugenini lakini, haipaswi kuwafanya wajiamini kupitiliza. Wanapaswa kucheza kwa adabu hasa Ugenini. Mechi inayofuata Kimataifa ya Yanga ni dhidi ya Al Ahly. Sio mechi rahisi japo Yanga anacheza nyumbani.

Tumewaona Al Ahly wakisumbuana na Simba kwenye mechi mbili hivi karibuni. Bado haipaswi kuwafanya Yanga wajiamini kupitiliza. Al Ahly ndiyo bingwa mara nyingi Afrika wa michuano hii.

Unapaswa kucheza naye kwa adabu. Kama Yanga wataona wanammudu kirahisi, yanaweza kujirudia yale mabao ya Algeria. Ukifungwa mechi mbili mfululizo, presha inakuwa juu. Matumaini ya kusonga mbele yanapungua. Ndiyo mpira ulivyo. Ukiwatazama Al Ahly msimu huu ni kama uwezo wao kidogo umepungua lakini Simba ni Simba tu. Hawazi kuwa swala. Yanga wana timu nzuri. Yanga wana wachezaji wazuri. Kujiamini kupitiliza kunaweza kuwaponza tena. Al Ahly wanafungika na hasa wanapokuwa ugenini lakini wanahitaji kuheshimiwa. Kuwashambulia tu kuwa na mipango mizuri ya kujilinda, wanaweza kukufunga nyingi tu nyumbani kwako. Kule Algeria nahisi kila Mwana Yanga alikuwa na kujiamini kupitiliza. Kuanzia viongozi, benchi la ufundi, wachezaji hadi mashabiki. CR Belouizdad sio KMC. Klabu Bingwa Afrika sio mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga wamekuwa wakicheza vizuri sana bila mpira lakini kule Algeria walikuwa unga sana. Walishindwa kumzuia Mwarabu kwenye mashambulizi ya kushitukiza. Karibu Mabao yote yalikuja kwa mtindo mmoja. Tuliwaona Al Ahly hapa wakicheza dhidi ya Simba. Ndiyo aina ya mpira wao pia wanapokuwa ugenini.

Yanga wanaweza sana kumiliki mpira kutokana na aina ya wachezaji walionao lakini wanapaswa kutojisahau. Kule Algeria walikuwa wanaenda wengi kushambulia na idadi ndogo ya wachezaji wanabaki kujilinda. Ukikutana na wapinzani wajanja, unaweza kufungwa nyingi. Kwa mtu ambaye hakutazama mchezo wa Yanga na CR Belouizdad, unaweza kudhani Yanga ilizidiwa sana. Sio kweli. Haikuwa hivyo hata Kidogo. Yanga ilimiliki mchezo, Belouizdad ikamiliki matokeo. Ndiyo ukatili wa mchezo wa soka. Haijalishi umepiga pasi ngapi, soka ni mchezo wa mabao.

Kwa timu ambayo haijacheza hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa miaka 25, haipaswi kujiamini kupitiliza. Kufunga Simba 5-1 kusiwadanganye. Kucheza fainali ya kombe la shirikisho msimu uliopita, kusiwatie jeuri. Ukiniuliza kwanini walifungwa 3-0 kule Algeria, nitakujibu hawakuwa na adabu kwa mpinzani wao.

Chanzo: Mwanaspoti