Hawaeleweki tu wameshaamua hawataki kueleweka, mara Jonas Mkude amiliki dimba la Kirumba kama yeye ndie Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameamua tu tusiwaelewe mara Joseph Guede atokee kwenye mechi muhimu tu, alitokea dhidi ya Belouzdad, akaja dhidi ya Mamelodi na leo kwenye operation Kirumba amezima Uchambuzi mwingi tu.
Hawaeleweki tu Wananchi, mara Gift Fred auwashe Beki wa pembeni wakati alisajiliwa kama Beki wa kati, mara Clement Mzize asieleweke kama anacheza Tisa ama kivuli, mara asitake kufunga zaidi ya kupika tu! Stephen Aziz Ki ndio kabisa simuelewi mara aje chini kama Mkabaji mara abaki juu kama false 9 mara acheze na anaweka kamba yake ya kideo, simuelewi tu na ana mabao 14.
Siwaelewi Wananchi, ghafla akaingia Kibwana Shomari, kumbe Mudathir nae alikuwa bench mara Zawadi Mauya mara akaingia Farid Mussa, siwaelewi kabisa Wananchi hivi hawana uchovu? Mara walisafiri mpaka Cairo, mara wakacheza mechi za Ligi Kuu, mara Pretoria na baadae Dodoma na leo Mwanza na bado hawajachoka siwaelewi kabisa.
Wamecheza kombe la CRDB bila Pacome Zouzoua na Kouassi Yao Yao na siwaelewi ni kama hakuna kilichotokea maana Aucho aliingia tu kupasha misuli, wamecheza leo kombe la NBC bila Pacome na Zouzoua, siwaelewi zaidi maana Kouassi ameshapona na hawajataka kumtumia, siwaelewi kabisa Wananchi!
Haya baada ya kutozielewa sana timu nyingine kuwa hazina zinachofanya ule wakati wetu umefika sasa, sijui tutaelewana??
Wamesalimu amri.