Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamchunge huyu dogo, ni hatari kwenye nyavu

Leonel Wamba Djouffo.jpeg Yanga wamchunge huyu dogo, ni hatari kwenye nyavu

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leonel Wamba Djouffo (21) raia wa Cameroon huyu ni mshambuliaji hatari zaidi kwenye kikosi cha CR Belouizdad ya Algeria.

Wamba alikuwa mwiba kwenye michuano ya AFCON Under 17 mwaka 2019 ambapo Cameroon walibeba ndoo yeye akiwa mshambuliaji kinara kabla ya kutimkiaSpartaks Jūrmala ya Latvian kisha kwenda Beloizdad.

Hadi sasa nyota huyu amefunga mabao matatu ndani ya CAF Champions League msimu huu akicheza dakika 90 tu, yaani kila baada ya Dakika 30 ana uhakika wa kufunga bao.

Kwenye mfumo wa 4-3-3 ambao CR Belouizdad hupenda kuutumia nyota huyu hucheza mbele ya Ishak Talal Boussouf (Boussouk + Wamba =⚽).

Wamba ana kasi kubwa miguuni, nguvu na maarifa makubwa kwenye boksi la mpinzani, urefu wake wa futi 6.1 unamwezesha kufunga kirahisi mipira ya juu.

Boussouf na Wamba wamekuwa tishio kwa mabeki wa timu pinzani Kwa sababu hawasimami eneo moja hali inayo wafanya walinzi wa timu pinzani wapate wakati mgumu kupambana nao.

Yanga dhidi ya timu za Algeria ndani ya miaka 10

19/6/2016 MO Bejaia 1-0 Yanga❌

13/8/2016 Yanga1-0 MC Alger✅

0/4/2017 MC Alger 4-0 Yanga❌

6/5/2018 USM Alger 4-0 Yanga❌

19/8/2018 Yanga 2-1 USM Alger✅

28/5/2023 Yanga 1-2 USM Alger❌

6/5/2023 USM Alger 0-1 Yanga✅

Yanga wamecheza mechi 5 na kushinda zote

TP Mazembe 0-1 Yanga

Rivers Utd 0-2 Yanga

Marumo 1-2 Yanga

USM Alger 0-1 Yanga

Al Merreikh 0-2 Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live