Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wamchunge huyu Mbrazil wa Mameldoi ni hatari

Sundowns New Signing Lucas Ribeiro Costa.png Yanga wamchunge huyu Mbrazil wa Mameldoi ni hatari

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya soka ya Yanga wanatarajia kushuka Dimbani, Machi 30, 2024 kumenyana na miamba ya soka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali ya CAFCL utakaopigwa katika Dimba la Mkapa majira ya saa 3:00 usiku.

Mamelodi wanafahamika kuwa mwiba kwa timu nyingi za Afrika kutokana na form yao nzuri kwa sasa, kuwa na wachezaji wazoefu na wenye uwezo mkubwa, benchi bora la ufundi chini ya kocha Rhulan Mokwena bila kusahau uwekezaji mkubwa walioufanya mabingwa hao wa mashindano ya AFL.

Mbali na hayo yote, Yanga wanapaswa kujua kuwa Mamelodi wana mchezaji mmoja hatari raia wa Brazil anayeitwa Lucas Ribeiro Costa (25), huyu nyota wa kuchungwa hasa na safu ya ulinzi ya Yanga, hapa nazungumzia kina Mwamnyeto, Bacca, Job na na viungo wakabaji kina Aucho na Mudathir.

Kitakwimu, Costa ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji au second striker (namba 10), katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini msimu huu wa 2023/24

Costa amecheza mechi 13, amefunga mabao 10 na kutoa assists 2 na ndiye kinara wa upachikaji mabao kunako Ligi Kuu ya PSL nchini Afrika Kusini mpaka sasa.

Top scorers Ligi ya Africa kusini

1. Lucas Ribeiro - mabao 10 - assists 2

2. Khanyisa Erick Mayo - mabao 9 assists 0

3. Bradley Grobel - mabao 8 assists 0

Msimu huu Peter Shalulile raia wa namibia hana maajabu sana kwenye ufungaji wa mabao ndani ya Ligi hiyo na hata kwenye Klabu ya Mamelodi.

Takwimu za Shalulile katika Ligi kuu Afrika kusini msimu huu wa 2023/24, amecheza mechi 13, amefunga mabao 3 na kutoaa assists 2. Ameanza katika mechi 11 zingine mbili amecheza akitokea benchi.

Kwa Yanga wao wanaye kiungo mshambuliaji, Aziz KI ambaye ndiye kinara wa upachikaji mabao kwenye Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 13 na assist 7 na anayemfuatia ni Feisal Salum (Azam FC) mwenye mabao 13 na aasists 5.

Kama wachezaji hao watakuwa fit Machi 30 basi huenda walinzi wa timu zote mbili wakapitia wakati mgumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: