Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waliwazidi hapa Dodoma Jiji

Okrah Aziz Mzize Yanga waliwazidi hapa Dodoma Jiji

Thu, 11 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi ambayo ilikuwa ya kupishana sana, kuanzia firimbi ya kwanza Kocha Baraza alijua kupata matokeo dhidi ya Yanga inapaswa "Alternate" nao, lakini Yanga walifanya Counter Pressing ambazo ziliharibu shape ya ulinzi ya Dodoma Jiji, why?

1: Dodoma Jiji walikabiwa juu zaidi na Yanga kitu ambacho kiliwapa shida kumove haraka kutoka eneo moja kwenda lingine, kwa kesi hii Yanga waliweka presha sana na walifanikiwa.

2: Hasa dakika 45 za kwanza Yanga waliweka pressure kwenye lango la Dodoma kwa kukabia juu, Dodoma Jiji walijikuta wakifanya mistakes za kupiga pass vibaya ambazo ziliwin na KI Aziz, Mzize, Okrah.

3: Dodoma Jiji walikuwa wanapiga pasi fupi fupi za haraka ili kupata space zilizo wazi za Yanga, lakini Yanga wakiwa hawana mpira 4-4-2 iliwapa faida ya kuwa na idadi ya wachezaji wengi kwenye mistari ya Kiungo na Ulinzi.

4: Dodoma Jiji wakiwa na mali wanakuwa 3-2-5 kuna wakati waliweza kusukuma mashambulizi kwenye lango la Yanga lakini maarifa ya kuipangua safu ya Ulinzi ya Yanga, uwepo wa Nzengeli uliwapa shida sana safu ya Kiungo cha Dodoma Jiji kwenye kutafuna space: Yanga waliset distance ndogo sana kwenye mistari yote mitatu (Ushambuliaji, Viungo, Ulinzi)

Kuna wakati Dodoma Jiji walikuwa wanafanya mistakes nyingi na kushindwa kufanya recovering vizuri, Yanga hawakuwa ruthless golini nafikiri hapo Dodoma Jiji walishukuru hilo.!

NOTE

1: Bacca ni beki bora bora sana , kumpita ni ngumu sana ( inawezekana lakini itakupa shida)

2: Kipagwile alikuwa na game nzuri sana

3: Aucho amerudi uwanjani, nimeona control ya mchezo kwa Yanga ilikuwa kubwa sana.

4: Mtenje alisema Yanga haiwezi kufunga magoli mawili, sijui anajisikiaje?

5: Robo fainali kwa Yanga ileee .!

6: Ukuta wa Yanga ni mgumu sana

FT: Dodoma Jiji 0-2 Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live