Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga walipofuzu mara ya mwisho nilikuwa shule - Arafat Haji

Gsm Hersi Arafati (22).jpeg Diamond Platnumz

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji amesema kuwa wakati Klabu hiyo ikifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya mwisho mwaka 1998 yeye alikuwa akisoma shule.

Arafat amesema kuwa alikuwa na mapenzi makubwa na klabu hiyo na leo ametimiza ndoto ya kuipeleka tena kwenye makundi ya Ligi hiyo akiwa kama makamu wa Rais, nafasoi ya juu kabisa ya uongozi ndani ya klabu.

Yanga imetinga hatua hiyo baada ya kuitoa Al-Merrikh ya Sudan baada ya kuifunga kwa mabao 3-0.

“Kutoka mwaka 1998 hadi sasa [2023] ni miaka 25, ni umri wa kijana ambaye tayari anaweza kuwa kwenye ndoa. Ni miaka mingi sana, wakati Yanga inacheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya mwisho mimi nilikuwa bado nipo shule.

“Mapenzi ya Yanga yalikuwa ndani ya familia yetu, nakumbuka siku hiyo mzee na familia yote tulishangilia sana Yanga kufuzu hatua ya makundi. Kwa hiyo Yanga kufuzu hatua ya makundi baada ya miaka 25 ni zawadi kwa familia yangu kwa sababu hata wao walitamani kuiona tunairudisha Yanga hatua hizi.

“Na mimi nimefurahi sana kuona jambo hili limetimia, tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha hatua hizi tunakuwa wenyeji kwa kushiriki kila msimu,” amesema Arafat Haji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live