Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga walipaswa kushuka daraja msimu huu - Mchambuzi

Yanga Imara Zaidi.jpeg Yanga walipaswa kushuka daraja msimu huu - Mchambuzi

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa Mujibu wa Kanuni ya 68 (3) ya Ligi Kuu inasema (Klabu ambayo itawasilisha Maombi yake ya usajili wa wachezaji wake ikiwa na upungufu ya wachezaji 20 Kwa timu yake au itakayopata uthibitisho wa wachezaji pungufu ya wachezaji 18 Kwa timu zake za vijana itakuwa imepoteza sifa ya kuwa Klabu ya Ligi Kuu.

Tarehe 26 Oktoba, 2023 Kulipaswa kuwepo na mchezo wa Ligi Kuu ya U20 baina ya Simba Sports dhidi ya Yanga Africa. Lakini Kwanini mechi haikuchezwa?

Ipo hivi,Kabla ya Mechi Simba Sports waliiandikia Barua TFF kuwataarifu Kutokuwa tayari kuchezwa mchezo huo kwasababu Yanga Africa hawakuwa wamesajili team yao ya U20 ambayo ni kiunyume Cha taratibu.Hapa kama Kawaida TFF wakaomba Busara itumike mchezo usichezwe.

Mzee wa Jambia niliendelea Kutafuta taarifa juu ya hili Jambo .Nikapata taarifa kutoka Chanzo Cha Kuaminika kuwa Kumbe Yanga Africa walipeleka TFF Majina ya team yao ya U20. Kama ni hivyo kwanini usajili wao kwenye Mfumo wa CAF na FIFA haupo??

Kuna vitu viwili Inawezekana vimetokea hapo.Inawezekana Yanga Africa walipeleka Majina kwa Kuchelewa na Kukuta tayari Mfumo umefunga. Au Meneja wa TMS ambae ni Meneja pia wa Idara ya Mashindano ya TFF alisahau Kuthibitisha Majina Kwenye Mfumo.

Lakini kama Yanga Africa ndo walikuwa Wana Makosa Kwa maana walichelewa kupeleka Majina kwanini TFF waombe Busara itumike na sio Kanuni? Hapa unagundua mtu mzima TFF ndo mwenye Makosa Kaomba kuchutama.

Taarifa zilizonifikia ni kuwa Kwa sasa TFF wanaandaa leseni Maalumu kwaajili ya wachezaji wa Yanga ili waweze tu Kushiriki Ligi msimu huu.Lakini Sasa unajiuliza vipi kuhusu mechi ambayo wameshacheza? Na Ina maana si walicheza Bila leseni?

Yanga Africa Mechi yao ya kwanza ambayo ni haramu walicheza dhidi ya KMC na Matokeo yalikuwa ni sare ya 2-2. Vipi kuhusu mechi zao za NBCPL ambazo pia ni haramu kwasababu Kwa Mujibu wa Kanuni hawakutakiwa Kushiriki Ligi msimu huu.

Hivi ni vitu vya Aibu na Fedheha kutokea kwenye Ligi inayojinasibu kama Ligi Namba 5 Kwa Ubora Barani Africa.Ni lazima watu kuwajibika au Kuwajibishwa.

Sijui itakuwaje iakini nitakuwepo this I WILL PROMISE YOU Barbra @mzeewajambia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live