Kuna wakati unahitaji wachezaji waweze kukusimamia kwa ustadi wa hali ya juu kushinda mipambano yao dhidi ya mpinzani aliyeimara sana , ndicho walichofanya wachezaji wa Yanga kuweza kumsimamia Miguel Gamondi kwa dakika 120 na kushinda mechi, kwa nini?
1: Wachezaji wote walikuwa karibu karibu sana iliwasaidia sana kuweka presha kwenye mpira wakipoteza (counter pressing), na hii kusaidia kudumisha mashambulizi (sustain attack)
2: Waliamua kuufanya uwanja kuwa mpanza ili kumtanua mpinzani wao zaidi (Ihefu), kwasababu alicheza nyuma na kupiga (lowblock)
3: Walikuwa na idadi ndogo ya pasi ndefu ndefu bali walitumia sana one touch football ili kumove safu ya Ulinzi ya Ihefu , repeatedly walifanikiwa sana
Ihefu wamepoteza mechi lakini wamefanya vitu vingi kwa usahihi , na kwa wakati sahihi : waliacha distance ndogo sana kwenye mstari yote mitatu na hii iliwapa faida kuzuia na kushambulia kwasababu walikuwa karibu karibu sana
YANGA wanabadilika sana , ukiweza kushinda mipambano yao kwa kiasi katika basi watabadilisha kutafuna spaces zilizo wazi pembeni (jinsi goli lilivyopatikana).
Kumbuka;
1: Yule Tanimu ni beki mzuri sana, wala hapaniki na wala hahofii kujaribu tena
2: Aucho kuna vipass fulani hivi alikuwa anapiga, mithiri ya Iniesta
3: Ondogo ni bonge la beki, energy nzuri sana
4: KI Aziz kwenye mita 25 ya mwisho ya uwanja ni hatari sana , anafunga tu
5: Zouzoua ni game changer wa maana kabisa
6: Energy na strength ya Attohoula Yao
FT: Ihefu FC 0-1 Young Africans.