Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wakizubaa kwa Bamako, ni kifo mbele ya TP Mazembe

Kocha TP Mazembe Kocha wa TP Mazembe, Pamphil Mihayo

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga wakijiandaa kuivaa Real Bamako ya Mali Machi 8 Jijini Dar es Salaam mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Basi wana kila sababu ya kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo sambamba na kuweka wigo wa alama baina yao na waliopo chini yao hususan TP Mazembe.

Yanga ambao wana alama 4 mpaka hivi sasa baada ya kucheza michezo mitatu iwapo watashinda mchjezo dhidi ya Bamako watakuwa na alama 7 na hivyo matokeo ya angalau sare watakapokwenda Lubumbashi yatakuwa na faida kwa upande wao

Na hiyo ni kutokana na kauli ya Kocha wa TP Mazembe ambao nao wako katika wingu zito la kufuzu kwa hatu ya Robo fainali baada ya kukubali kupoteza michezo miwili kati ya mitatu waliyocheza mpaka hivi sasa.

Akizungumza Kocha Pamphil Mihayo wa TP Mazembe anasema;

“Tumejiweka katika mazingira magumu, kuna nidhamu tuliipoteza dhidi ya Monastir, kama Yanga wakishindwa kuwafunga Bamako tunaweza kukimbizana kwa kuwa sisi na wao tutakutana hapa kwetu hiyo itakuwa ni Fainali ambayo Mungu atakuwa ametuletea.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live