Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wakikutana na Ihefu wanateseka - Mchambuzi

Mudathir Yanga Musonda Yanga wakikutana na Ihefu wanateseka - Mchambuzi

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa, kikosi cha timu ya Yanga kinapokutana na Ihefu Fc kazi huwa ni ngumu kwa Yanga kupata matokeo.

Wakanda amesema hayo kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya timu hizo utakaopigwa leo huko highland Estates, Mbrarali Mbeya huku Yanga ikiwa na kumbukumbu ya Ihefu kuivunja unbeaten yao ya mechi 49 msimu uliopita.

"Tangu Yanga aanze kukutana na Ihefu FC mwaka 2019 wamekuwa wakipata mechi ngumu sana Yanga. Kwenye ligi kuu msimu uliopita Ihefu dhidi ya Yanga mechi zote mbili ziliisha kwa kugawana alama tatu tatu.

"Ihefu akiwa Mbarali Highland Estate alimfunga Yanga goli 2-1 na Yanga alipokuwa kwa Mkapa alifunga goli 1-0, kwahiyo ukiangalia ni mechi mbili ambazo zilikuwa na intensity kubwa," Wakanda Republic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live