Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wakifungwa leo ni uchovu - Master Tindwa

Yanga Wakifungwa Leo Ni Uchovu   Master Tindwa Yanga wakifungwa leo ni uchovu - Master Tindwa

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka nchini Master Tindwa amesema, endapo itatokea leo Yanga SC atapotezwa mchezo wa leo basi uchovu utakuwa umechangia.

Akizungumza jana kwenye uchambuzi wake Clouds FM, mchambuzi huyo alisema kikosi cha Yanga hakijasambaratika kutoka kile cha msimu uliopita hivyo uchovu pekee labda ndio utakaochangia.

“Kama Yanga watapoteza mchezo wa kesho (leo) uchovu utakuwa umechangia sana lakini kikosi kilichofika fainali hakijasambaratika na sitashangaa kwa sababu hata msimu uliopita walianza ugenini wakafungwa, lakini hawakufungwa tena hadi kwenye fainali hapa kwa Mkapa," alisema Master Tindwa.

Yanga wanatarajia kushuka dimbani usiku wa leo kucheza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi ya CAFCL huko nchini Algeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live