Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wakibugi tu wanatoka kapa msimu huu

Yanga Mapinduzi Fg Yanga wakibugi tu wanatoka kapa msimu huu

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waswahili walipata kusema "kuchamba kwingi mwishowe utashika kinyesi" na wengine wakaenda mbali zaidi wakasema" Safari za sakafuni huishia ukingoni".Hivyo ndivyo unaweza sema.

Ni kama Yanga wameanza kujisahau na kulewa sifa kwa kile walicho kitengeneza misimu kazaa iliyopita.

Ni kawaida kabla ya msimu klabu hukaa chini na kujiwekea malengo yake. Moja ya lengo kubwa kwa timu kubwa ni pamoja na kutwaa mataji.

Hicho kitu kwa Yanga naona kama kinaenda kupotea pengine wao kwa mtizamo wao wanaona wapo kwenye mstali bado.

Narudia tena Target ya timu kubwa ni kuchukua mataji na si kutafuta nafasi ya kubaki mashindanoni kama ilivyo kwa timu nyingine ndogo.

Kwa sasa ni kama klabu ya Yanga imeanza kupoteza focus na mission zao zinaonekana zinakwama.

Taji la pili sasa limepitwa kushoto mpaka sasa inaelekea nusu msimu kutamatika bado wanayanga hawaoni hilo.

Wao bado wamelala wakati wapinzani na mahasimu wao wakuu wanaenda kumaliza mission zao na ninadhani moja ya malengo ya Simba ni kuchukua taji la Mapinduzi huku ikiwa tayari ina Ngao ya jamii kabatini.

Baada ya Mapinduzi Cup kuisha na pengine Simba ikafanikiwa kutwaa, ndio sasa tutaona na kuskia zile hesabu za 5-2 zinaanza kupigwa.

Kwa kawaida msimu shiriki huwa na mashindano kuanzia 5 na yakizidi ni ziada, hivyo kila timu inajuwa msimu ujao plan zake nikufanya nini.

Kwa haraka haraka mpaka sasa Yanga imepoteza.

❌Ngao ya jamii ❌Mapinduzi Cup ↪CAFCL ↪FA Cup ↪NBC league

Pengine kufanikiwa kumfunga mtani ndilo lengo lao kubwa...yaani wamelewa sifa mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: