Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waja kivingine

Yanga Yangaaaaa Yanga wakiendelea kujifua

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Uongozi wa Yanga umepanga kuja na mikakati mipya itakayowapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo.

Msimu huu, Yanga tayari imecheza michezo miwili ya ligi ambayo yote wamefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli, amesema kuwa moja ya mkakati waliouweka msimu huu ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo wa ugenini.

Bumbuli amesema kuwa lengo ni kupata pointi tatu katika kila mchezo, hilo linawezekana kutokana na usajili bora walioufanya msimu huu.

“Tumekuja na mpango mkakati ambao wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wanafahamu, kikubwa ni kufanikisha malengo yetu ya msimu huu.

“Hatutaki kuacha pointi yoyote tunapokuwa ugenini ambako kuna viwanja vibovu. Hatutaki kurudia makosa tuliyoyafanya msimu uliopita. tukipata pointi tatu ugenini basi na nyumbani hatutaki kuacha pointi yoyote,” amesema Bumbuli.

Chanzo: globalpublishers.co.tz