Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waitana kwa Mkapa kumnyoa Mamelodi

Yanga Mashabiki 232 Mashabiki wa Yanga

Sat, 30 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka Yanga; Mwananchi, ile siku ya kuipa heshima nchi yetu imefika ambapo leo, kikosi cha timu yetu ya Young Africans SC kitashuka dimbani kumenyana na Mamelodi Sundowns, ukiwa ni mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo uliopewa jina la Muda Day wenye kauli mbiu isemayo ‘SIMU ZIITE, TUKUTANE KWA MKAPA’, utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 usiku.

Mapema jana, Kocha Mkuu, Miguel Gamondi, aliuzungumzia mchezo huo akisema: “Unapohitaji kufika madaraja ya juu ya soka la Afrika lazima ucheze dhidi ya miamba ya Afrika. Mechi hii ya Mamelodi ni changamoto nzuri sana. Kwangu huu umekuwa msimu mzuri sana, tumecheza na Al Ahly na sasa Mamelodi.”

Tiketi za mchezo huo bado zinauzwa, hivyo Mwananchi fanya haraka kuwahi tiketi yako, ili tuwe pamoja katika sehemu ya kuweka historia na heshima huku tukiwa tumeujaza uwanja.

Ikumbukwe kwamba, mpaka sasa, Tiketi za Royal na V.I.P A zimemalizika, zilizobaki ni za V.I.P B ambazo ni Tsh 20,000 na V.I.P C zinazouzwa Tsh 10,000. Usisahau kuwa, Jukwaa la Mzunguko hakuna kiingilio, yani ni BURE!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live