Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu wa 2023/2024 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.
Prisons ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Benno Ngassa dakika ya 4 tu ya mchezo huo lakini furaha yao haikudumu kwani dakika 6 baadaye yaani dakika ya 10 Aziz Ki aliisawadhishia Yanga kwa free-kick baada ya kufanyiwa faulo kabla ya kufunga bao la pili dakika moja baaye (dakika ya 11).
Mpaka mapumziko ubao ulisoma Yanga 2-1 Prison, lakini mapema kipindi cha Pili Kennedy Musonda aliiandikia Yanga bao la tatu dakika ya 59 baada ya shambulizi ambalo Aziz Ki alikosa bao.
Dakika ya 79, Aziz KI alishindilia msumari wa mwisho na kuvuruga hesabu za Tanzania Prison na hata mpinzani wake Fei Toto ambaye walikuwa wakiwania naye kiatu cha ufungaji bora na kumfanya Aziz aongoze akiwa amefunga mabao 21 na fei mabao 19.
Full Time|
Simba 2-0 JKT Tanzania
Yanga SC 4-1 Tz Prisons
Geita Gold 0-2 Azam FC
Singida FG 2-3 Kagera.
Mashujaa 3-0 Dodoma
Namungo 3-1 Tabora Utd
Coastal Union 0-0 KMC
Ihefu 5-1 Mtibwa Sugar.
#NBCPL: Goli la kwanza la Yanga limewekwa nyavuni na Aziz Ki
— Azam TV (@azamtvtz) May 28, 2024
Yanga 2-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’ / Ngasa 4’)
LIVE #AzamSports3HD
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #SokaLetuDamdam #MechiNaneLIVE #MechiZoteLIVE #AzamTV #EndOfSeason pic.twitter.com/IVcjve11Qo
#NBCPL: Chuma ya 20 kwa Stephane Aziz Ki
Yanga 2-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’ / Ngasa 4’)LIVE #AzamSports3HD
— Azam TV (@azamtvtz) May 28, 2024
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #SokaLetuDamdam #MechiNaneLIVE #MechiZoteLIVE #AzamTV #EndOfSeason pic.twitter.com/xu4eV4HtDS
#NBCPL: Chuma ya tatu kwa Yanga ikiwekwa nyavuni na Kennedy Musonda.
— Azam TV (@azamtvtz) May 28, 2024
Yanga 3-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’, Musonda 52’ / Ngasa 4’)
LIVE #AzamSports3HD
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #SokaLetuDamdam #MechiNaneLIVE #MechiZoteLIVE #AzamTV… pic.twitter.com/4bhuYShI7d
#NBCPL: Goli la 21 kwa Aziz Ki na ni hat trick yake ya pili msimu huu.
— Azam TV (@azamtvtz) May 28, 2024
FT: Yanga 4-1 TZ Prisons (Aziz Ki 11’, 12’, 79’, Musonda 52’ / Ngasa 4’)
LIVE #AzamSports3HD
#NBCPremierLeague #LigiKuuYaNBC #NBCPL #NBCPLUpdates #SokaLetuBambam #SokaLetuDamdam #MechiNaneLIVE… pic.twitter.com/PWKoO0sd7T