Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waishangaza TP Mazembe kwa Mkapa

Yanga 3 1 Mkapa.jpeg Yanga imeshinda 3-1 mbele ya TP Mazembe

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Timu ya Yanga imeibuka na ushindi wa magoli 3-1 mbele ya TP Mazembe ya Congo mchezo wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo wa kundi D umewashuhudia Yanga waliokuwa katika kiwango bora kabisa wakitakata katika Uwanja wa Mkapa tangu dakika ya mwanzo ya mchezo.

Magoli ya Yanga katika mchezo wa leo yamefungwa na Kennedy Musonda na Mudathir Yahaya kipindi cha kwanza kabla ya winga Tuisila Kisinda kupachika bao la tatu dakika za lala salama.

Goli pekee la TP Mazembe limefungwa na Ngonga kwa mpira wa adhabu na kumshinda mlinda mlango wa Yanga Djigui Diarra.

Mpaka dakika 90 zinakamilika ni Yanga ndio walioibuka wababe huku mchezo mwingine wa kundi hilo ukimalizika kwa sare kati ya Real Bamako dhidi ya US Monastir.

Mpaka sasa msimamo wa kundi D ni kama ufuatao

1. US Monastir — 4pts 2. TP Mazembe — 3pts 3. Yanga SC — 3pts 4. Bamako — 1pt

Chanzo: www.tanzaniaweb.live