Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waifuata Geita Gold CCM Kirumba

Skudu Diarra Aucho Yanga waifuata Geita Gold CCM Kirumba

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga, kimesafiri jana saa 3 usiku kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi ya wiki hii, Oktoba 7, 2023 majira ya saa 10 jioni kwenye dimba la CCM Kirumba. Hii ni baada kupoteza mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu kwa goli 2-1.

Kikosi kimesafiri na wachezaji 23 sambamba na viongozi wa benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Wachezaji waliosafiri ni; Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Joyce Lomalisa, Kouassi Attohoula Yao na Nickson Kibabage.

Wengine ni Khalid Aucho, Zawadi Mauya, Salum Abubakar, Mudathir Yahya, Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki na Jesus Moloko.

Katika msafara huo, pia wapo Kennedy Musonda, Clement Mzize, Mahlatse Makudubela, Hafiz Konkoni, Denis Nkane, Fred Gift, Crispin Ngushi na Kibwana Shomari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: