Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waichapa Simba Nusu Fainali Ngao ya Jamii, uso kwa uso na Azam Fainali

Yanga Vs Simba 1 0 Yanga waichapa Simba Nusu Fainali Ngao ya Jamii, uso kwa uso na Azam Fainali

Thu, 8 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imefanikiwa kutinga Fainali ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya watani, Simba katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 44 akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo.

Sasa Yanga watakutana na Azam FC katika Fainali itakayopigwa Jumapili hapo hapo Uwanja wa Mkapa kuanzia Saa 1:00 usiku ikitanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu itakayoanza Saa 10:00 jioni.

Azam FC imetinga Fainali kwa ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Mabao ya Azam yamefungwa na winga Mgambia Gibril Sillah dakika ya 13, kiungo Feisal Salum dakika ya 40, washambuliaji Mcolombia Jhonier Blanco dakika ya 45'+1, Adam Omary dakika ya 87 na kiungo Mcolombia, Ever William Meza Mercado dakika ya 90'+2.

Kwa upande wao, Coastal Union ambayo itakutana na Simba Jumapili jioni, mabao yao yamefungwa na kiungo Charles Semfuko dakika ya 27 na Abdallah Hassan dakika ya 85.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: