Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waichapa Red Arrows kilele cha "Wiki ya Mwananchi" kwa Mkapa

Mudathir X DUBeeeee Yanga waichapa Red Arrows kilele cha

Mon, 5 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Yanga imetoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika mchezo wa kirafiki leo kuhitimisha tamasha la kilele cha Wiki ya Mwananchi usiku wa Jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Red Arrows, mabingwa wa mwaka huu Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati walitangulia kwa bao la mshambuliaji Ricky Banda dakika ya sita, kabla ya viungo, mzawa Mudathir Yahya Abbas kusawazisha dakika ya 62 na Mburkinabe Stephane Aziz Ki kufunga la ushindi dakika ya 90’+3 kwa penaltı.

Huo unakuwa mchezo wa nne kwa Yanga katika maandalizi yake ya msimu mpya baada ya awali kucheza mechi tatu kwenye kambi yake ya Afrika Kusini, ikishinda 4-0 dhidi ya Kaizer Chiefs na 1-0 dhidi ya TS Galaxy kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mechi ya kwanza na Augsburg ya Ujerumani.

Yanga sasa inarejea kambini Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 8 hapo hapo Uwanja wa Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: