Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waichapa Mbeya City kibabe wakiendelea kuweka rekodi

Khalid Aucho DR Yanga waichapa Mbeya City kibabe wakiendelea kuweka rekodi

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Timu ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika Dimba la Benjamin Mkapa wakiichapa Timu ya Mbeya City magoli 2-0.

Magoli ya Yanga katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji hatari Fiston Mayele, kipindi cha kwanza akiweka wavuni bao moja huku bao la pili akifunga kipindi cha pili.

Kwa kutopoteza mchezo wa leo, inaweongeza rekodi nyingine kwa Yanga ambapo wanacheza mchezo wa 49 wa Ligi Kuu pasipo kupoteza.

Kwa ushindi wa leo Yanga wanaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC wakifikisha alama 32 baada ya michezo 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live