Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waichapa Geita Gold goli 3, Maxi Nzengeli wa moto

Yanga 3 Vs Geita 0 Yanga waichapa Geita Gold goli 3, Maxi Nzengeli wa moto

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Timu ya Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Wachimba dhahabu wa Geita Gold katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mchezo huo wa mzunguko wa Tano ulikuwa na ushindani mkubwa huku Yanga wakifanya jitihada kubwa kusaka goli baada ya kutoka kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Ihefu.

Mabao ya Yanga katika mchezo wa leo yamefungwa na Pacome Zouzoua, Aziz KI na Maxi Nzengeli ambae alionesha kiwango bora katika mchezo wa leo.

Kwa ushindi huo Yanga inafikisha alama 12 na kusogea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi akimshusha Simba mwenye alama 12 kwa idadi ya magoli ya kufunga huku Simba akiwa amecheza michezo minne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live