Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waichapa Dodoma Jiji Jamhuri, Mayele mambo bado

Ambundo Dickson Master Mchezo umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 mbele ya Dodoma Jiji

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakiwa ugenini katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Dodoma Jiji na kufanya waweze kukusanya alama tatu.

mabao ya Dickosn Ambundo dk ya 11 na bao la pili la kujifunga kwa kipa wa Dodoma Jiji, Mohamed Yusuph dk ya 35 katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Zawadi Mauya jambo lililomfanya ajifunge.

Kinara wa mabao ndani ya Yanga, Fiston Mayele amemaliza mechi ya nne hii leo pasipo kupachika bao lakini amesema kuwa yeye kutokufunga sio tatizo kikubwa ni ushindi wa timu.

“Nimekuwa nikipata nguvu ya kuendelea kupambana licha ya mabeki kuweza kunikamia wakitaka nisiweze kutetema kwenye mechi ambazo wanacheza wanahitaji nisiteteme.

“Ushindi wa timu ni kitu cha msingi kisha mimi ninakuwa na kazi ya kutimiza majukumu yangu hasa kwa malengo ambayo ninakuwa nimejiwekea,” amesema.

Yanga inafikisha pointi 60 ikiwa imecheza mechi 24 ndani ya Ligi Kuu Bara aa haijapoteza mchezo mpaka sasa.

Kiungo wa Dodoma Jiji, Hassan Nassoro aliweza kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa dk ya 88 kwa kumchezea faulo Yannic Bangala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live