Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waichapa Bamako kwa Mkapa, Robo Fainali kiulaini tu

Yanga Vs Bamako Mkapa Yanga sasa wanahitaji alama tatu tu kufuzu hatua ya Robo Fainali

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kimefanikiwa kuchukua alama tatu muhimu mchezo wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo wa kundi D, umewashuhudia wawakilishi hao wa Tanzania wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Bamako kutoka nchini Mali.

Mabao ya Yanga katika mchezo wa leo yamefungwa na Fiston Mayele kipindi cha kwanza akipokea pasi safi kutoka kwa Kennedy Musonda na Jesus Moloko kipindi cha pili baada ya makosa ya walinzi wa Real Bamako.

Kwa ushindi huu wa leo Yanmga wanafikisha alama 7 na kuendelea kukamata nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi D. Na ushindi huu ni kama unakwenda kurahisisha harakati za Yanga kufuzu hatua ya Robo Fainali.

Msimamo wa kundi D

1. US Monastir — 10pts

2. Yanga SC — 7pts

3. TP Mazembe — 3pts

4. Bamako — 2pts

Chanzo: www.tanzaniaweb.live