Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waichapa Azam FC Mkwakwani! Aziz Ki, Mzize hatari na nusu

Yanga Vs Azam 2 0 FT.jpeg Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao dhidi ya Azam FC

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la Azam na Ngao ya Jamii, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii usiku huu Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Yanga imetumia dakika 5 tu kuamua mchezo huo kwa mabao ya kiungo mshambuliaji, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 85 na Clement John Mzize dakika ya 89.

Wawili hao wote walifunga baada ya kutokea benchi kwa pamoja dakika ya 62, Aziz Ki akichukua nafasi za Crispin Ngushi na Mzize nafasi ya Farid Mussa.

Aziz KI hilo ni bao lake la pili kuifunga Azam FC ambapo bao lake la kwanza aliwafunga katika mchezo wa Ligi msimu uliopita.

Gamondi ameanza msimu mpya wa rekodi nzuri akishinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Azam huku mpinzani wake Yusuf Dabo akipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga

Kipa wa Yanga Djigui Diarra amefanikiwa kutoka kwenye dakika 90 za pili dhidi ya Azam bila kuruhusu bao mechi zote zikichezwa Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.

Yanga sasa imeingia Fainali ambayo itachezwa Jumapili na itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya pili kesho baina ya Simba SC na Singida Fountain Gate hapo hapo Mkwakwani Saa 1:00 usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: