Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wafunga busta, Mayele, Fei Toto wakoleza mzuka

Mayele Feitoto Yanga Yanga wafunga busta, Mayele, Fei Toto wakoleza mzuka

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vibqra wa Ligi Kuu Bara, Yanga wanaendelea kujifua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi zijazo za duru la pili, huku mzuka ukiongezeka kwa kurejea kwa baadhi ya mastaa wao na mabosi wametamba leo watafunga busta dhidi ya Polisi Tanzania ya Kocha Mwinyi Zahera.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Polisi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku kocha mkuu, Nasreddine Nabi aliyekuwa akitumikia adhabu ya mechi tatu akirejea kikosini na mastaa Fiston Mayele, Feisal Salum ‘Fei Toto’ waliokosa mechi za kufungia ungwe ya kwanza na ile ya Kombe la ASFC.

Wababe hao walioifumua Kurugenzi ya Simiyu mabao 8-0 bila kuwepo kwa Nabi benchini na wachezaji hao, imepanda mchezo wa kesho kuingiza mziki wote ili kuinyoosha Polisi.

Ili kuanza kwa kishindo duru la pili, Yanga imewarejesha mazoezini mastaa wake wote akiwemo Mayele mwenye mabao 10 kikosini hapo na Feisal waliopumzishwa kwenye mchezo wa ASFC uliopigwa Desemba 11.

Pamoja na mastaa hao kurejea, jambo lingine jema kwa Yanga ni kurejea kwa kocha Nabi aliyekuwa akitumikia adhabu.

Ikumbukwe mara ya mwisho Nabi kukaa kwenye benchi la Yanga ilikuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu, ikichapwa 2-1, na baada ya hapo timu iliongozwa na Kocha Mrundi Cedric Kaze katika mechi tatu akianza na Tanzania Prisons, dhidi ya Namungo na ule wa Kombe la Shirikisho, hivyo adhabu ya Mtunisia huyo imeisha na sasa rasmi ataivaa Polisi.

Urejeo wa Nabi kikosini hapo ni mwendelezo wa maandalizi ya timu hiyo kufanya vizuri kwani hata alipofungiwa alikuwa akiendelea kukinoa kikosi hicho mazoezini na wiki hii Yanga imekuwa ikifanya mazoezi ya aina mbili, kwa nyakati tofauti ambayo ni yale ya utimamu wa mwili yanayofanyika ‘gym’ na uwanjani sambamba na yale ya mbinu na namna ya kucheza mechi dhidi ya Polisi ambayo imepania kushinda.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema kikosi kizima kimeendelea vyema na mazoezi na kila kitu kipo sawa kwa ajili ya mechi ijayo inayotarajiwa kuwa ngumu.

“Wachezaji na benchi zima la ufundi wameendelea na programu za mazoezi kwa ajili ya mechi zijazo.

Mazoezi yanayofanyika ni yale ya gym na mbinu na kila kitu kwa upande wetu kipo katika hali nzuri kwa ajili ya mechi na Polisi.” alisema Walter.

Kocha Kaze amefunguka waliwapumzisha baadhi ya mastaa wao dhidi ya Kurugenzi ili kuhakikisha wanakuwa fiti katika mchezo wa Polisi.

“Yanga ina wachezaji wengi na bora, hivyo ili kila mmoja aonyeshe uwezo wake inatulazimu kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya mechi,” alisema Kaze na kuongeza;

“Wengi ambao haukuwaona dhidi ya Kurugenzi siyo kama wana matatizo au majeruhi tuliwapumzisha kwa ajili ya mechi zijazo.”

Yanga inaongoza ligi ikiwa na alama 38 katika mechi 15 za duru la kwanza ikishinda 12, sare mbili na kupoteza moja tu, huku Polisi Tanzania ikiwa mkiani na alama tisa tu, baada ya kushinda michezo miwili tu na sare tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live