Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waendelea kuburuza mkia kundi D, watatoboa?

Medeama Vs Yanga FT Mchezo umemalizika kwa sare ya goli 1-1

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shughuli katika dimba la Baba Yara, Khomas Ghana, Wananchi wanaendelea kusubiri ushindi wa kwanza kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo uliowakutanisha Yanga dhidi ya mwenyeji Medeama umemalizika kwa sare ya goli 1-1.

Wenyeji Medeama ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo kwa mkwaju wa penati dakika ya 26 likiwekwa wavuni na Sowah ( P) 26’ kabla ya Pacome Zouzoua kuwarudisha Wananchi mchezoni kwa bao la kusawazisha dakika ya 36.

Katika mchezo mwingine wa kundi D, Vinara Al Ahly wamelazimishwa sare ya bila kufungana na CR Belouizdad.

MSIMAMO KUNDI D

1. Al Ahly (pointi 5)

2. Medeama (Pointi 4)

3. CR Belouizdad (Pointi 4)

4. Yanga SC (Pointi 2)

Kuna tofauti ya alama tatu kati ya kinara Al Ahly ya Misri na washika mkia Young Africans SC, bado nafasi ipo.

Je una maoni gani kutokana na msimamo wa kundi D? Tuachie Commeny yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: