Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga wacheze kama Simba kwa Al Ahly - Mchambuzi

Simba, Yanga Waanza Kuweka Viporo Mechi Za NBC Yanga wacheze kama Simba kwa Al Ahly - Mchambuzi

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini na mtangazaji wa EA Radio, Ibra Kasuga amewaonta Yanga SC kuhusu mbinu yao ya kufungua turbo na kwenda kushambulia wote kwenye lango la mpinzani, na badala yake kuweka mpango mkakati wa kujilinda ili wasifungwe kwa mashambulizi ya kushitukiza.

Kasuga amesema hayo kuelekea mchezo mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo Yanga watatupa karata yao ya pili keshokutwa Jumamosi, Desemba 2, dhidi ya Al Ahly baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Kasuga amewataka Yanga kucheza kama Simba kwa tahadhari ya kujilinda na kutafuta nafasi za kushambulia kwa tahadhari kama ambavyo Simba wamekuwa wakifanya wanapokutana na timu kubwa za Afrika.

"Yanga huwa anai-commit timu yote kwenda foward, wanaacha space....wanaacha watu wachache nyuma...wanapigwa counter attack watu wanafunga magoli ambayo kwa haraka haraka unaweza ukasema yalikuwa ni magoli mepesi lakini strategically CR Belouizdad walijua ni namna gani wanaweza wakawapiga Yanga"

"Ndio maana nasema hata huyo Al Ahly ambaye amekuja hapa Tanzania amekuwa akifungwa na Simba wakati mwingine akitoka sare na Simba ni kwa sababu huyo Simba kuna eneo ambalo alikuwa ana-balance.

"Simba alivyokuwa anamfunga Al Ahly ulikuwa unaona Defensive & Attacking walikuwa Well Balanced, maana yake nachotaka kusema ni kwamba Yanga kwa ubora wake huu huu atakapokuja hapa akitokea akafungua Turbo akashambulia sana.

"Kama hatacheza kwa nidhamu ya Ku-Balance kushambulia na Kujilinda Al Ahly ana watu ambao kwenye nafasi mbili tatu akakuumiza," amesema Ibra Kasuga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live