Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Vital'O yahamishiwa Chamazi

Aziz Ki Maxi Ssada Yanga vs Vital'O yahamishiwa Chamazi

Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klabu ya Yanga Sc, Eng. Hersi Said amethibitisha kuwa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Vital’O ya Burundi utapigwa katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ulipochezwa mchezo wa awali.

Mchezo wa pili utapigwa Jumamosi, Agosti 24, 2024 baada ya ule wa kwanza Yanga kuibuka na ushindi wa bao 4-0.

“Kutokana na marekebisho yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mkapa, mechi yetu ya marudiano dhidi ya Vital’O, hatutacheza tena uwanja wa Mkapa, Tutacheza katika uwanja wa Azam Complex, Jumamosi majira ya saa 1:00 jioni.

“Mechi iliyopita wenzetu Vital O walisema watatunywa kama supu lakini tulifanikiwa kupata ushindi wa Goli 4, Lakini kwenye mchezo huu wa marudiano ni zamu yetu sasa kuwanywa wao kama supu,” amesema Eng Hersi Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live