Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Tabora United kupigwa Mei Mosi CRDB Cup Federation

Yanga Diarra Aziz Ki Wachezaji wa Kikosi cha Yanga mazoezini

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi, Yanga SC watamenyana na Tabora United Mei 1 katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano ambayo sasa inajulikana kama CRDB Bank Federation Cup Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuanzia Saa 2:30 usiku.

Mchezo huo utatanguliwa na michezo miwili siku hiyo ya Robo Fainali ya CRDB Bank Federation Cup kati ya Ihefu SC na Mashujaa Saa 10:00 jioni Uwanja wa LITI mjini Singida na Coastal Unión dhidi ya Geita Gold Saa 12:15 jioni Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Hatua ya Robó Fainali ya CRDB Bank Federation Cup itakamilishwa Mei 3 kwa mchezo kati ya Azam FC na Namungo FC Saa 1:00 usiku Uwanja Azam Complex.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: