Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs TP Mazembe; Ni kumbukumbu na kisasi

Bangala, Aucho N Mayele Yanga vs TP Mazembe ni mechi ya kumbukumbu na kisasi

Sat, 18 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Siku ya Jumapili Wananchi watafurika uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe. Mchezo huo utapigwa saa 1 usiku.

Ni mechi ambayo itakuwa na kumbukumbu tofauti kwa mashabiki wa Yanga.

Kwanza ni kurejea kwa aliyekuwa kiungo wao pendwa Mukoko Tonombe ambaye alijiunga na TP Mazembe katika dirisha dogo la usajili msimu uliopita.

Mukoko aliitumikia Yanga mwaka mmoja na nusu uliopita akiwa mmoja wa wachezaji waandamizi.

Hata hivyo baada ya usajili mkubwa uliofanywa na Yanga kuepekea msimu wa 2021/2022 mukoko alikumbana na wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kocha Nasreddine Nabi.

Baadae Yanga iliamua kumtumia katika makubaliano ya usajili wa winga Chiko Ushindi aliyetoka Mazembe kuja Yanga na Mukoko kujiunga na Mazembe.

Dabi ya Congo itahamia kwa Mkapa Ikumbukwe kuwa Dabi kubwa ya Congo DR ni kati ya TP Mazembe na AS Vita. Wachezaji wengi wa Yanga ukiachana na Watanzania, nazungumzia wa Kimataifa wanatoka Congo na wengi wao wamecheza AS Vita. Ukianza na Fiston Mayele, Djuma Shaban, Jesus Moloko, Yanick Bangala, Joyce Lomalisa, Tuisila Kisinda wote hawa wamecheza AS Vita.

Kwa hiyo Dabi waliokuwa wakiipiga Congo na TP Mazembe sasa wanaihamishia kwa Mkapa, safari hii wakiwa Yanga. Kwa hiyo inazaliwa Dabi nyingine kati ya Yanga na Mazembe kutokana na upinzani mkubwa wa wachezaji wa AS Vita na Mazembe.

Jumapili itakuwa mara ya kwanza kwa Mukoko kukutana na waajiri wake hao wa zamani.

Lakini pia hii ni mechi ya kisasi kwa Yanga, timu hizi zilikutana kwenye michuano hii mwaka 2016 wakati huo hatua ya makundi ikiwa ikiwa na timu nane tu, Yanga Yanga ikipangwa kundi A na timu za Mo Bejaia, TP Mazembe na Medeama.

TP Mazembe waliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo ambao uliibua kipaji cha winga Juma Mahadhi ambaye hata hivyo majeraha yaliathiri muendelezo wa kipaji chake.

Wananchi wanakumbuka katika mchezo huo, aliyekuwa mwenyekiti wakati huo Yusufu Manji aliwalipia mashabiki wote viingilio na hivyo uwanja wa Mkapa kujaa ilipofika saa 5 asubuhi.

Wananchi wengi walijitokeza kushuhudia mchezo huo lakini wakakumbana na mabomu ya machozi baada ya jaribio la kuvunja geti ili waingie uwanjani.

Kwa hakika itakuwa mechi ya kipekee na Mwananchi hakikisha umenunua tiketi yako mapema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live