Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Namungo kupigwa Septemba 20

Yanga Pacome Nzengeli  Djbout Pic Yanga vs Namungo kupigwa Septemba 20

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeupangia tarehe husika mchezo wa Yanga SC wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo ambao sasa utachezwa Septemba 20, 2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, saa 1:00 Usiku.

Mchezo huo wa raundi ya tatu, awali haukupangiwa tarehe kutokana na timu yetu kuwa na majukumu ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh utakaochezwa Septemba 16, 2023 nchini Rwanda.

Ikumbukwe kuwa, timu ya Yanga SC, ndiyo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ikikusanya alama 6 baada ya kucheza mechi mbili na kushinda zote, huku ikifunga magoli 10, hatujaruhusu goli lolote.

Kuanza vizuri kwa msimu huu 2023-2024, ni ishara njema kwa kikosi hicho kuelekea kutetea ubingwa wa ligi hiyo ambao wameuchukua mara 29 ikiwa ni nyingi zaidi kuliko timu zote shiriki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live