Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Mamelodi: Gamondi akoshwa na wachezaji wake

Maxi Yangaa (29).jpeg Yanga vs Mamelodi: Gamondi akoshwa na wachezaji wake

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

GAMONDI achekelea uwezo wa wachezaji wake

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa amefurahishwa na utendaji wa kazi wa wachezaji wake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Machi 30 ubao wa Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali baada ya dakika 90 ulisoma Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilianza mchezo huo ikiwa na mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha kwanza wakikosa huduma ya profesa Pacome, Yao Yao ambao hawa hawakuwa fiti.

Gamondi amesema: "Nimefurahishwa na uwezo wa wachezaji wa timu yangu kwa kuwa kila mmoja alijitoa kwenye kutimiza majukumu yake licha ya kwamba kuna nafasi ambazo tulishindwa kuzitumia.

"Bado kuna nafasi ya kufanyia kazi makosa kwa kuwa kuna mchezo mwingine ambao tutacheza dhidi yao, tuna matumaini yakufanya vizuri mchezo ujao,".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live