Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs JKT Tanzania, naziona bao 5-0 alizopigwa KMC - Baraka Mpenja

YANGA KIMATAFA M Kikosi cha Yanga

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wa Mabingwa Watetezi,Yanga SC unaofuata ni dhidi ya JKT Tanzania maafande hawa ambao ndio mabingwa wa Championship kwa msimu uliopita kama ilivyo kuwa kwa Yanga.

Ni mechi ya Mabingwa Watetezi siku ya tarehe 29,si ya kukosa kabisa ni mwendo wa burudani kwa wananchi na mashabiki wa Yanga SC.

Nilibahatika kuangalia mchezo wa Kwanza wa ligi ya NBC kwa upande wa JKT TANZANIA dhidi ya Namungo FC ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0 kwa uzembe wa golikipa wa Namungo, Nahimana.

JKT Tanzania wapo na wachezaji wengi ambao wana uzoefu na ligi ya NBC lakini hawana Quality ya Kusumbua Yanga wachezaji kama Daniel Lyanga, Dilunga, Ndemla, Makka Edward, David Bryson na wengineo wengi wametemwa kwenye vilabu vyao na walikuwa hawapati nafasi ya kuanza na huku ndio tegemezi.

Kwa Quality ya Yanga SC sasa na nikiitazama JKT iliyocheza dhidi ya Namungo naziona zile goli 5 kama kwa KMC Juzi japo mpira haupo hivyo labda kocha Malale Hamsini aje na Nidhamu kubwa mbele ya Yanga SC asitake kushindana na Yanga Kama Kocha Moalin wa KMC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: