Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Coastal Union, kuna 'Sapraizi' leo?

Coastal Vs Yanga Leo Mkwakwani Yanga vs Coastal Union, kuna 'Sapraizi' leo?

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu ya NBC inaendelea tena leo Jumatano Novemba 8, 2023 kwa mchezo mmoja Coastal Union V/s Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga kuanzia majira ya saa 12:30 jioni

Coastal Union ipo katika nafasi nne za mwisho [nafasi ya 13] ikiwa na alama saba kwenye msimamo wa Ligi, wameshinda mchezo mmoja tu kati ya nane ambayo wameshacheza hadi sasa wakiwa wamepoteza michezo mitatu huku wakitoka sare katika michezo minne.

Ukiachana na msimu uliopita, Coastal Union ilikuwa ikiisumbua sana Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga! Baada ya Yanga kutegua mtego huo, tunasubiri kuona leo itakuwaje?

Yanga ndio vinara wa Ligi kwa sasa, wameshinda michezo saba kati ya nane waliyocheza, Wananchi wamefunga magoli 25 huku wakiwa wamefungwa magoli matano.

Yanga inaingia kwenye mchezo huu kama timu inayopewa nafasi kubwa ya kushinda mbele ya Coastal Union kwa sababu ya ubora wa kikosi, mwenendo wa matokeo ya mechi zilizopita n.k

Wakati mwingine timu za madaraja ya kati zinapokutana na timu zinazowania ubingwa wachezaji wanahamasika zaidi ukiachilia mbali mbinu na ufundi kutoka benchi la ufundi.

Baada ya Yanga kutoka kwenye mchezo mkubwa ambao wachezaji walitumia nguvu nyingi na hawajapata muda wa kutosha kupumzika, natarajia kuona Gamondi akifanya mabadiliko kwenye baadhi ya maeneo.

Wananchi bado wapo kwenye kilele cha furaha ya ushindi wa 5G mbele ya mtani wao, je wataendelea walipoishia Jumapili?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: