Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Azam: Watu wa kazi waingia chimbo

AYOUB LYANGA (600 X 380) Watu wa kazi waingia chimbo

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikiwa zimebaki siku sita kabla ya Mzizima Dabi kupigwa ndani ya Uwanja wa Azam Complex, mastaa wa Azam FC ikiwa ni pamoja na Prince Dube, Ayob Lyanga, James Akamiko, Idd Suleiman, (Nado) wanapewa mbinu kuikabili Yanga.

Mastaa hao wanasukwa chini ya Kocha Mkuu, Yusuph Dabo aliyetoka kukiongoza kikosi kusepa na pointi tatu ugenini dhidi ya Coastal Union, kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Timu zote mbili zinakwenda kukutana zikiwa na uwiano sawa kwenye orodha ya mabao ya kufungwa ambayo ni mawili, tofauti Azam FC kipa Idrissu Abdulai alitunguliwa bao mojamoja kwenye mechi mbili tofauti huku Djigui Diarra akitunguliwa mabao yote mawili mchezo mmoja dhidi ya Ihefu.

Ni Yanga pekee ina hasira ya kupoteza pointi tatu mazima dhidi ya Ihefu ikikusanya jumla ya pointi 12 kwenye mechi tano huku Azam FC ikiwa haijapoteza mchezo na kibindoni ina pointi 13.

Dabo ameweka wazi kuwa kila baada ya mchezo wanafanyia kazi makosa ili kuwa tayari kwa dakika 90 zinazofuata kwenye mechi zao zote.

“Kila baada ya mchezo tunaanza maandalizi ya kupata pointi tatu kwa mechi inayofuata. Wachezaji wanajituma na makosa yanayoonekana kwenye mechi husika tunafanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi,”.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 22, Uwanja wa Azam Complex.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live