Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs Azam Fc ilikuwa ajenda ya siri

Vita Vita Yanga Vs Azam Azam FC vs Yanga

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ile ajenda ya siri iliyokuwa ikisubiriwa kwenye kufungua zawadi za Christmas kati ya Azam FC na Yanga, iligota ukingoni baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Azam FC 2-3 Yanga.

Hapa Spoti Xtra linakuletea baadhi ya matukio yaliyotokea kwenye msako wa pointi tatu katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa juzi Jumapili.

KWENYE MTEGO WA KUOTEA

Ilikuwa ni kwa Azam FC ambao walikuwa wakimtumia Prince Dube kwenye eneo la ushambuliaj, alionekana katika eneo hilo dakika ya 21 alipokuwa akilifuata lango la Yanga.

Kwa upande wa Yanga, Jesus Moloko alionekana kwenye eneo la kuotea dakika ya 26 na 66, Fiston Mayele alionekana kwenye mtego wa kuotea dakika ya 44.

MASHUTI AMBAYO HAYAKULENGA LANGO

Prince Dube alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 5, 58, 66, Keneth Muguna dakika ya 15, huku Abdul Sopu akifanya hivyo dakika ya 23. Kwa upande wa Yanga ni Mayele dakika ya 69.

MASHUTI YALIYOLENGA LANGO

Sopu alipiga mashuti dakika ya 12, 30, 14, 27, 47, mabao yalikuwa dakika ya 27 na 47, kwa upande wa Yanga ni Mayele alipiga mashuti yaliyolenga lango dakika ya 31 ambapo lilikuwa ni bao na Stephane Aziz Ki alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 76 kwa pigo la faulo na alifunga bao moja dakika ya 32. Farid Mussa alipiga shuti dakika ya 77 ambalo lilikuwa ni bao la tatu na ushindi kwa Yanga.

MAPIGO YA FAULO

Kwa Azam FC walikuwa wakimtumia Dube kwenye upigaji faulo, alifanya hivyo dakika ya 11 kwa Yanga ni Aziz Ki alipiga faulo dakika ya 4 na 76.

WALIOCHEZA FAULO NA KUCHEZEWA

Bernard Morrison alicheza faulo dakika ya 17, 26, 61 alipewa kazi ya kupiga faulo dakika ya 50. Aziz Ki alichezewa faulo dakika ya 35. Mayele alicheza faulo dakika ya 75, alichezewa faulo dakika ya 2 na 9. Joyce Lomalisa alicheza faulo dakika ya 6, Dickson Job alicheza faulo dakika ya 6

Khalid Aucho alichezewa faulo dakika ya 54, Muguna alicheza faulo dakika ya 35, Sospeter Bajana alicheza faulo dakika ya 2, 76. Dube alichezewa faulo dakika ya 10, Sopu alichezewa faulo dakika ya 5. James Akaminko alichezewa faulo dakika ya 26 na 54, alicheza faulo dakika ya 62.

MAPIGO YA KONA

Kipre Junior alipiga kona kwa upande wa Azam FC dakika ya 11, 16, 43 na 44. Aziz Ki alipiga kona dakika ya 83, Morrison dakika ya 24.

WAMWAGA KROSI

James Akaminko alipiga krosi dakika ya 51, Lusajo Mwaikenda alipiga dakika ya 4, 14, 45 na 85, Dube alifanya hivyo dakika ya 8.

Lomalisa alipiga krosi dakika ya 10, 19, 51 na 83, Mayele dakika ya 16, Kibwana Shomari dakika ya 6 na 62, Aziz Ki dakika ya 16 na 18, Morrison dakika ya 23, 25 na 37.

KADI ZA NJANO

Bajana alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 76, Sure Boy alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 53, Yannick Bangala alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 59, Djigui Diarra alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 87.

SUPER SUB

Farid Mussa wa Yanga alikuwa ni nyota wa mchezo kwa kuwa aliingia dakika ya 73 akichukua nafasi ya Morrison ambaye alitoa pasi moja ya bao.

Farid alifunga bao la ushindi dakika ya 77 lililoipa pointi tatu Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live