Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga vs ASAS FC kupigwa Chamazi Complex

Yanga Mwed Ngao Yanga vs ASAS FC kupigwa Chamazi Complex

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitendo cha Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwa katika matengenezo kimefanya mchezo wa awali wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga SC na ASAS ya Djibouti kupigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Yanga SC watacheza mchezo huo Jumapili katika uwanja huo ulioko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“ Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha Wanahabari na mashabiki wetu wote kuja katika mchezo huo ambao tunataka kuutumia kutuma Salamu kwa wapinzani wetu.

“Tutacheza mchezo wetu wa kwanza hatua ya awali CAFCL dhidi ya ASAS kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi 20.08.2023 majira ya saa 11:00 jioni" amesema Ali Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live