Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ukiwakamata hawa tu unamaliza mechi

Pacome Maxi Aziz Ki Yanga ukiwakamata hawa tu unamaliza mechi

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga msimu huu mpaka sasa ni wazi imekuwa ikibebwa na ubora wa safu ya viungo washambuliaji, ambao viungo hao wamekuwa na uwezo wa kucheza mpira vizuri na kufunga pale inapobidi.

Yanga ina kwenda kushindana kwenye michuano ya ndani na ya kimataifa, na inaonesha wazi kuwa safu ya ushambuliaji sio bora sana! Ukitazama namba za Konkoni, Mzize na Musonda utanielewa vizuri.

Point yangu ni nini? Point yangu ni kuwa siku Yanga atakapokutana na timu ambayo yeye ni first team inaweza kukusaidia sana kwa suala la shughuli za Viungo wao! Itawasadia sana, na itawapa matokeo easy.

Lakini Yanga ikikutana na timu ambayo uwiano unafanana au Wananchi wakawa ni second team na ukawa kutawala jumla, hapa ndipo wataona thamani ya mshambuliaji! Kuna mechi ambazo zitawalazimu kila mchezaji atimize majukumu yake ya msingi.

Kazi ya viungo sio kufunga bali kuifanya itoke kwenye presha na kutengeneza nafasi za magoli kwa washambuliaji, lakini ikiwa mpinzani yupo chini ndipo viungo huliendea jukumu la tatu! Huu ndio uhalisia kuhusu kazi ya Viungo.

Yanga kuna mechi ana kwenda kukutana nazo ambapo zitamlazimu kila mmoja atimize majukumu yake ya msingi kwa asilimia mia, hapo Yanga watashinda vipi mipambano yake? Ni swali ambalo linasalia.

Kuna mahala Yanga watafika wataliona gape hili la kutokuwa na safu nzuri ya ushambuliaji, ingwaje ni miongoni mwa timu zilizofunga magoli mengi msimu huu! Dirisha likifunguliwa waende sokoni mapema sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: