Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo wana hamu kubwa ya kushuhudia kandanda safi kutoka kwa wachezaji wao na kutinga hatua ya makundi ambayo wamekuwa wakiisikilizia kwa miaka 25 sasa bila mafanikio.
Kamwe amesma hayo jana wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa keshokutwa Jumamosi, Septemba 30, 2023 dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan katika Dimba la Azam Complex.
Katika mchezo wa kwanza, Yanga wakiwa ugenini nchini Rwanda walifanikiwa kushinda kwa bao 2-0, hivyo wanahitaji sare ya bila kufungana au sare ya bao 1-1 tu ili waweze kutinga makundi ya CAFCL.
"Ukitaka kujua wana Yanga wana ugwadu na huu mchezo, tayari baadhi yao wameshaingia kwenye mfumo kuangalia tiketi, Tayari baadhi ya mashabiki wameshanunua tiketi kupitia mfumo kabla ya sisi kutangaza mfumo hadharani.
"Sisi sio Klabu namba tatu kwa ubora wa Afrika kwa bahati mbaya, ni lazima tuonyeshe hilo kwa kutinga hatua ya makundi. Hivyo hizi tiketi zinaweza kuisha mapema mno kama shabiki hutanunua tiketi mapema," amesema Ally Kamwe.