Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga sasa wahamishia nguvu Kimataifa wikiendi hii

Yanga Sasa Wahamishia Nguvu Kimataifa Wikiendi Hii.png Yanga sasa wahamishia nguvu Kimataifa wikiendi hii

Mon, 12 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baaada ya kuchukua ubingwa wa Ngao ya Jamii, Yanga SC sasa akili yao inahamia Kimataifa ambapo wikiendi hii Agosti 16, 2024 wanatarajia kukipiga na Vital'O ya Burundi.

Yanga ambao wamesajili vizuri kuongezea nguvu kikosi chao ambacho msimu uliopita kilifika Robo Fainali na kutolewa na Mamelodi kwa mbinde, safari hii wana ndoto za kufika mbali zaidi.

Akizungumza mara baada ya kutwaa Ngao ya Jamii jana Agosti 11, 2024 dhidi ya Azam FC, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema safari hii wamedhamiria kufika mbali zaidi kutokana na usajili walioufanya.

"Msimu uliopita tulitolewa Robo Fainali, msimu huu malengo yetu ni kufika mbali zaidi, watu walishangaa kwa nini tumemsajili Boka wakati tulikuwa na Joyce Lomalisa ambaye alikuwa bora lakini tukamleta bora zaidi na mmemuona lengo ni kufanya vizuri zaidi," alisema Injia Hersi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live