Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga sasa ni master Manu Labota, Moloko ndiyo hivyo

Manu Labota Yanga sasa ni master Manu Labota, Moloko ndiyo hivyo

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mwanspoti linajua kwamba Yanga kwenye dirisha dogo hili la usajili wanamleta winga mpya mwenye makali na hesabu zao ziko kwa Manu Lobota Bola ambaye ni staa wa FC Lupopo ya DR Congo.

Timu hiyo ni watani wa jadi wa TP Mazembe pale jijini Lubumbashi. Bola ni mmoja kati ya mawinga bora waliobaki nchini Congo kwasasa akiwa staa mkubwa ndani ya klabu yake. Anasifika kwenye kutengeneza nafasi na hata kufunga mabao makali.

Mwanaspoti linajua mchezaji huyo tayari amefanya mazungumzo ya siri na mabosi wa juu wa Yanga na kilichobaki ni kumalizana na klabu yake ya Lupopo kwa kuweka fungu mezani.

Hesabu za Yanga zinaweza kuwa rahisi kumnyakuwa Bola kutokana na ukaribu wa tajiri wa Mabingwa hao wa Tanzania, Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ na Rais wa Lupopo, Jacques Kyabula Katwe.

Lakini hata miaka ya nyuma Yanga waliwahi kuchukua mastaa kama Patrick Katalay na Pitchou Congo kwenye klabu hiyo na wakatamba mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Katwe ndiye gavana mwenye ushawishi kwasasa wa Jiji la Lubumbashi akiwa kwenye hesabu za kugombea muhula wa pili wa uchaguzi unaoendelea nchini humo ambaye pia ana mawasiliano mazuri na GSM.

Hata hivyo, Lupopo haitalegea kirahisi kumuachia Bola kutokana na ndiye staa mkubwa katika timu hiyo akicheza sambamba na mshambuliaji Mtanzania George Mpole.

Kama Yanga itamnasa Bola basi kuna uwezekano mkubwa wa kuachana na Jesus Moloko ingawa bado ana mkataba na timu hiyo.

Moloko amekuwa hana uhakika wa namba kwasasa ndani ya kikosi cha Yanga ambapo tangu atue kocha Miguel Gamondi anasotea benchi kwenye mechi nyingi.

Yanga inataka kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchezaji kikosini na akili zao zikiwa kutetea kombe lao na kupiga hatua kwenye michuano ya kimataifa ambako sasa wanasaka robo fainali.

Yanga pia inaye winga Skudu Makudubela ambaye hajawa na namba ya kudumu.

Chanzo: Mwanaspoti