Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga sasa ni full Kicheko, baada ya Aziz Ki hawa hapa wanaofuata

Yanga Vigogo Viongozi wa Yanga

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga wanacheka sana baada ya kusikia Simba imerudisha kasi ya kumsainisha mkataba mshambuliaji wa Asec Mimosas, Aziz KI na sasa wamehamishia mawindo kwa mashine nyingine mbili hukohuko Ivory Coast.

Yanga imekamilisha dili la Aziz KI na wanachopanga sasa ni lini mshambuliaji huyo raia wa Burkina Fasso atue nchini kusimamisha nchi.

Hata hivyo, bosi wao aliyekamilisha usajili huo, Injinia Hersi Said amebaki Ivory Coast akisaka mashine nyingine mbili mpya akiwamo beki na mshambuliaji wa mwisho.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ni kwamba Yanga sasa inasaka beki na mshambuliaji wa mwisho na Injinia Hersi leo atakuwa uwanjani kuangalia wachezaji hao wawili katika mechi ya Ligue 1 ya Ivory Coast itakayozikutanisha Asec Mimosas na Bassam.

“Tumeshatoka huko kwa Aziz KI sisi tunachoangalia sasa hesabu zingine. Hiyo ofa yao (Simba kwa KI) tulishaiona mapema kabla hata Injinia hajasafiri ndio maana tukaenda haraka kumaliza,” alisema bosi mkubwa ndani ya GSM ambao ni wafadhili wa Yanga ambao fedha zao zimerudisha hadhi ya mataji ndani ya klabu hiyo.

“Injinia bado yuko hukohuko tuna kazi zingine za kufanya pale Ivory Coast, kuna watu wawili bado nao tunawataka kama tutavutiwa nao. Hii Yanga ya msimu ujao kaka watu wajipange,” alisema kigogo huyo.

“CAF wanataka majina ya timu mapema ndio maana unaona mambo yanakimbia hakuna muda kabisa.”

Japokuwa kigogo huyo hakuitaja mechi ya leo, lakini Mwanaspoti linafahamu Hersi leo saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki atakuwa uwanjani kushuhudia mechi ya ligi ya nchi hiyo kati ya vinara wa ligi hiyo Asec dhidi ya Bassam inayoshika nafasi ya 10.

Inaelezwa klabu zote mbili Yanga inahitaji huduma ya mchezaji mmoja kutoka kwao baada ya kupata taarifa za ubora wao. Katika hatua nyingine, Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi jana alirejea nchini akitokea kwao Ubelgiji alikokwenda kwa mapumziko mafupi tayari kuendelea kumalizia msimu.

Tangu kusimama kwa Ligi Kuu Bara kupisha mechi za kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) Yanga imekuwa kwenye mazoezi makali chini ya kocha msaidizi Cedric Kaze huku ikitoa dozi nzito kwenye mechi mbili za kirafiki, ambapo jana iliifunga JKT Tanzania mabao 3-2 ilhali Jumanne iliyopita iliifunga Friends Rangers mabao 8-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live